Mawio au kupambazuka kwa jua eneo la likoni shelly beach.je kupambazuka kwa jua kila siku kunakupa taswira gani kama kiumbe?
Ni miaka mitano imepita sasa tangu nianzishe blog hii, nashkuru mwenyezi mungu kwa kunipa nafasi ya kuwa na afya njema mda wote huo mpaka kufikia leo ninapoandika tena kwenye blogi hii.
Nimeweka picha hii ya mawio kama ishara ya mwamko mpya ,kuashiria kuwa licha ya kuwa kimya mda wote huo bado niko na nia ya kuendeleza malengo yango ya kusoma na kuelimishana na wengine kupitia mtandao.
Kama munavyojua kuna ulimwengu na malimwengu.Ulimwengu na hii sayari tunayoishi sisi sote kama viumbe,na malimwengu na vitendo au yale yote yanayotusibu sisi kama viumbe.
Hii blogi nimeiita malimwengu kwa lengo la kujuzana mengi yanayo tuhusu au kutusibu kama waja wa mwenyezi mungu.Katika malimwengu kuna furaha,majonzi,njaa,shibe,uzima,ugonjwa na mengi mengineo ambayo twaweza kuyajadili.
sawa
ReplyDelete